tender details

TANGAZO LA ZABUNI

Tarehe: 17 March, 2023
1.Kituo cha Uhasibu cha APC Hotel and Conference Centre kinachotoa huduma ya hoteli na kumbi za mikutano kinatangaza zabuni ya utunzaji wa bustani katika kituo.
SN JINA LA ZABUNI NAMBA YA ZABUNI
1 UTUNZAJI WA BUSTANI APC/002/2022/2023/NC/03
2.Kituo cha Uhasibu cha APC Kinapenda kuwakaribisha waombaji wenye sifa kutuma maombi yao kwa ajili ya zabuni ya utunzaji wa bustani.
3. SIFA ZA MUOMBAJI: Muombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo
 • Awe Mtanzania
 • Muombaji awe ni Kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na ambayo haijawahi kuzuiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kujihusisha na shughuli za Ununuzi wa Umma.
 • Muombaji awe na mtaji wa kutosha ambao utamwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
 • Muombaji awe na leseni hai ya biashara inayoendana na zabuni atakayoomba.
 • Muombaji awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja wa kutoa huduma kulingana na zabuni atakayoomba.
 • Muombaji awe na cheti cha Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN)
 • Muombaji awe amesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) (kama ipo)
 • viii. Muombaji awe na hati hai ya kuthibitisha ulipaji wa kodi (Tax Clearance) (kama ipo)
 • Muombaji awe na uwezo wa kumbatanisha nakala za Proforma Invoice, Tax Invoice, Delivery Note na risti ya EFD.
 • Muombaji atatakiwa aambatanishe na kopi ya risti ya EFD ya hivi karibuni aliyowahi kutoa sehemu yeyote ya huduma.
 • Sifa ya nyongeza Muombaji awe na cheti cha OSHA, pia awe amesajiliwa kwenye Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
4. Zabuni zitashughulikiwa kwa utaratibu wa ushindani wa kitaifa [National Competitive Bidding] ulioainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013, zikisomwa pamoja na marekebisho yake ya Mwaka 2016 na ziko wazi kwa waombaji wote wa hapa nchini.
5. Waombaji wote wenye nia na uwezo wanaweza kupata taarifa kamili kupitia makabrasha ya zabuni katika ofisi ya Idara ya Manunuzi kwenye Kituo cha APC, kila siku kuanzia saa mbili kamili (02.00) asubuhi hadi saa kumi (16:00) kamili alasiri, siku za Jumatatu hadi Ijumaa [isipokuwa siku za sikukuu zinazotambulika kitaifa].
6. Muombaji atatakiwa kujaza kwa usahihi na kuwasilisha Fomu ya dhamana ya zabuni katika muundo wa (Bid Securing Declaration) inayopatikana kwenye kabrasha la zabuni.
7. Zabuni zote ziwe na nakala halisi (original) moja (1) na nakala (copies) moja (1) zinazofanana zifungwe ndani ya bahasha iliyofungwa kwa lakiri na juu ya bahasha ziandikwe maelezo ya Zabuni na kisha iandikwe na kuwasilishwa kwa anuani iliyoainishwa katika kabrasha la zabuni.
8. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya zabuni tarehe 03/04/2023 saa tano kamili (5:00) asubuhi,
9. Zabuni zitakazochelewa kuwasilishwa, zabuni za kielektroniki, na zabuni zisizofunguliwa katika tukio la ufunguaji zabuni, kwa hali yoyote ile hazitakubaliwa kwa tathmini.
..............................

IDARA YA MANUNUZI KITUO HOTELI NA KUMBI ZA MIKUTANO APC

Mawasiliano: 0714 40 53 80